SERIKALI imesema klabu ya Yanga haiwezi kupewa eneo la ziada kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wake wa kisasa wa soka.
Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji
Ofisa
Habari wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rehema Isengo
alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, tayari eneo la Jangwani liko
katika mipango ya maendeleo.
Msimamo
huo wa Wizara huenda ukawa pigo kubwa kwa Yanga, ambayo ilipanga
kujenga Uwanja wa kisasa katika maeneo ya Jangwani, Dar es Salaam.
Klabu
hiyo, juzi ilisitisha mkataba wa ujenzi wa uwanja huo na Kampuni ya
Beijing Contractors Engineering ya China, ikisubiri majibu ya barua yao
ya kupata eneo la nyongeza kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi.
Rehema
alisema katika mazungumzo ya awali kati ya Wizara na Manispaa, tayari
eneo la Jangwani liko kwenye mradi wa kujengwa City Garden, hivyo Yanga
haiwezi kupewa eneo hilo.
Alisema
Yanga ilishapewa majibu hayo kupitia ofisi ya Mipango Miji na kuongeza
kuwa, Wizara haihusiki na ugawaji wa viwanja kwa vile suala hilo lipo
chini ya Halmashauri.
Alisema
kazi ya Wizara ni kupitia faili lililowasilishwa kabla ya kutia saini.
Mbali na hilo, Rehema alisema Yanga inadaiwa deni la kodi ya Ardhi tangu
mwaka 1997 hivyo ameitaka kulilipa mara moja.
"Yanga
siyo walipaji wazuri wa kodi, wanadaiwa kodi tangu 1997, wameshapewa
maelezo wafuatilie na kulipa kodi hiyo,"aliongeza. Ofisa Habari huyo
aliweka wazi kuwa, athari inazoweza kupata Yanga endapo itashindwa
kulipa deni hilo ni kunadiwa kwa mali zake au kupelekwa mahakamani.
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto hakuwa tayari kuzungumzia suala
hilo jana. ------CREDIT LIWAZO ZITO BLOG.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment