BABA mzazi wa staa wa
sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu,
Balozi Abraham Isaac Sepetu ameagwa jana jioni nyumbani kwake Sinza -
Mori jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilihudhuria
na viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Jaji
Joseph Warioba, Getrude Mongela pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe na wengine wengi waliofika kutoa
heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia Jumapili ya
wiki iliyopita.
Waziri Membe kwa niaba ya
serikali ametoa salamu za rambirambi na kuchangia kiasi cha shilingi
milioni 1, “Kwa niaba ya serikali tumechangia kiasi cha shilingi
milioni 1. Hata mimi pia nilimfahamu marehemu kwa muda mrefu na alikuwa
kiongozi makini, Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi
amen,” alisema Waziri Membe.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa mazishi.
Mh.
Jaji Warioba akisaini kitabu cha Maombolezo leo mchana nyumbani kwa
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mh. Bernard Membe akisaini kitabu cha maombolezo leo October 29, 2013
nyumbani kwa marehemu Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Mama
Gertrude Mongella akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake Sinza Mori leo
October 29, 2013
Mh.
Jaji Warioba na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh.
Bernard Membe wakibadilishana mawazo kwenye msiba wa Marehemu Balozi
Isaac Abraham Sepetu leo October 29,2013
Baadhi ya viongozi waliofika msibani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Mtoto
mkubwa wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Aman Isaac Sepetu
akizungumza jambo na mwandishi wa habari, Mkwaia wa Kuhenga leo
October 29, 2013 nyumbani kwa Marehemu
Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu ukiwa ndani ya jeneza
Ndugu
na jamaa wakiuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo
nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment