Mac
Elvis alikuja Tanzania wiki mbili zilizopita kwa ajili ya consert Dar es
salaam akiwa na wasanii wenzake kutoka Uganda ambao walirudi baada ya
consert ila yeye akabaki ili kufanya kolabo na baadhi ya wasanii wa
Tanzania.
Mtanzania Gee ambae ni rafiki yake, anasema ‘Alhamisi
Elvis alikwenda kumtembelea rafiki yetu mmoja anaitwa Lulu (Sio
mwigizaji) anaishi Mbezi Beach Africana ambapo Ijumaa jioni mida ya saa
moja alijisikia kwenda kuogelea kwenye swimming pool, Lulu alimwambia
asiogelee kwa sababu ilikua usiku umeshaingia lakini Elvis aliiamua
kuogelea hivyohivyo’
‘Lulu alitoka nyumbani kidogo wakati huo Mac akienda
kuogelea akiwa mwenyewe, ilikua ni kawaida kwake kuogelea mara nyingi
huwa anapenda kuogelea hivyo hakikua kitu kigeni… Lulu aliporudi
hakumuona Mac manake hakurudi hivyo akadhani mwimbaji huyu ameshaondoka,
akawa anampigia simu rafiki anaeishi na Mac lakini haikupokelewa
‘Kesho
yake mida ya saa nne mlinzi ndio akaona nguo pembeni na aliposogelea
akaona mwili wa Mac ndani ya swimming pool chini ambapo baada ya
kutolewa alionekana akiwa na jeraha kwenye paji la uso hivyo inaonekana
alijigonga alipojirusha, tumbo lake halikujaa maji kama ambavyo
ilidhaniwa, tayari mipango ya kumsafirisha imekamilika na anapelekwa
kwao Uganda leo October 22 2013′
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment