Wassira aka Tyson alikuwa mpinzani namba moja wa wapinzani kwenda ikulu kuongea na rais kuhusu mswada wa katiba mpya akidai wanafuata chai na juisi za Ikulu na kuwa safari hii hawataitwa Ikulu.
Bila kuamini macho na masikio yake akashangaa kuona wapinzani wanatinga Ikulu na kufanya mazungumzo mazito na rais na kufikia makubaliano muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu.
Kwa ufupi Wassira anaonekana kuhusudu sana chai na juisi ndio maana aliona ni hoja muhimu kuliko katiba. Katika moja ya majukumu yake ya uwaziri ni pamoja na kujenga mahusiano mema lakini yeye mara nyingi amekuwa akitoa kauli za kufarakanisha badala ya kupatanisha. Kwa ufupi ni kuwa ameexpire kimawazo!
Source: Tanzania Daima 23/10/2013
Sasa ukiiangalia na kuitafsiri hiyo katuni, utaona wakati yeye Wassira anashughulika na chai na juisi rais pamoja na viongozi wa upinzani wako busy kwenye majadiliano. Sasa ukimuangalia yeye mhudumu usoni, ameshikwa na mshangao kwakuwa anaona anaowahudumia hawanywi chai wala juisi bali wanajadili hoja. Angalia vizuri hata kikombe cha rais kina chai lakini hanywi badala yake anaongoza majadiliano.
Kwakuwa aliokuwa anawahudumia hawakufuata chai na juisi inaonekana siku hiyo alivimbiwa kwani ni wazi viongozi hawa hawakuwa na muda wa kunywa chai na juisi kama alivyokuwa akidhani badala yake wakamwachia yeye!
via-- jamiiforums
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment