Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


 

 

Siku moja baada ya Boss wa Watanashati Ostaz Juma na Musoma kutangaza kuwa amemfukuza Janjaro kwenye kundi la watanashati kwa sababu za utovu wa nidhamu, C.E.O huyo ameamua kumrudisha tena kundini rapper huyo.
Ostaz Juma ameiambia tovuti ya Times fm  kuwa ameamua kumrudisha kundini Janjaro kwa kuwa ameonesha hali ya kuelewa na kumhakikishia kwamba amebadilika .


“Nimeamua kumrudisha, kwa sababu yale mambo yaliyopelekea mpaka mimi kutoa maamuzi yale niliyotoa jana, yaani kawa kama mtu mzima mwenye akili timamu, na mtu yeyote anayelifikiria na akaona kwamba hili ni kosa akasema kwamba ntajirudi, ni kumpa nafasi ya kumsikiliza.


“Kwa hiyo jana tulikaa kama kikao cha familia nyumbani kwangu, tukazungumza na ni kweli ameona kwamba ni bora aache baadhi ya mambo ambayo hayakuwa mazuri kwenye jamii, na mimi nachokitaka dogo Janja awe mtu bora, awe mzuri katika jamii. Na yeye ameniahidi kwamba, 


atawahakikishia watanzania kwamba atakuwa dogo janja ambae watanzania wanamtaka wao.” Amesema Ostaz Juma.
Janjaro ameiambia tovuti hii kuwa bado yuko watanashati na kwamba ile tofauti kati yao ilimalizika baada ya kikao.


“ Mi niko mtanashati, kwa sababu ni mambo ya kifamilia na tumeshakuwa familia moja, na mimi naona kuhamahama sio swala zuri, na kama nilikuwa na malengo ya kufanya kazi nzuri, ni bora niendelee kupalilia tu hapahapa. Yamekwisha isha kwa ufupi.”


Kuhusu wapi alikosea na anaona hatakiwi kurudia tena,janjaro amewatupia lawama 'marafiki' kwa kuwa chanzo cha yote.
“Kwa namna moja ama nyingine ni ile chuki, marafiki ambao wamenizunguka, ni watu ambao ni soo, sio watu wazuri. Sasa hivi  rafiki yangu hela tu.”


Janjaro na Ostaz Juma kwa pamoja wameahidi kuendelea kutoa burudani kwa fans wao,ambapo Ostaz amesema sasa hivi
amejipanga zaidi kama msanii na ataachia ngoma nyingi kali akiwa na wasanii wengine wa kundi la Watanashati.CHANZO TIMES FM

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top