Chidi
Benz alieleza sababu tatu kuu alizohisi zilimsukuma Nay wa Mitego
amdiss. Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi cha wiki iliyopita, Chidi
alisema baada ya kusikia diss ya Nay, aliamua kumchimba zaidi na
kugundua kuwa alikuwa akisikia nyimbo za Nay hata kabla hajajulikana kwa
Watanzania wengi.
“Kwanini kanidiss huyo mtoto,” Chidi alisema.
“Kwanini kanidiss huyo mtoto,” Chidi alisema.
“Design
yake kumbe hii, manondonondo, naye mhuni Manzese, na mimi ni Chidi
najulikana kwa story za kihuni, kwahiyo mpaka dakika hii amenidiss,
either maskani yao ashajipanga. Mbili kashajua kwamba siku tukikutana
kwenye show ‘labda Chidi akitaka kuniletea noma, na mimi nasimama
nioneshe watu kuwa mimi huniwezi wewe’. Tatu kanizingua kuna mtu ana
mchongo wake katika huu muziki kazinguana na mimi kalichukua ‘hilo
toto’ kaliambia ‘fanya hivi na hivi, imba sauti kama… fanya hivi beba
manondo, tembea kifua wazi ile kama mimi.. eeh unakuwa..halafu tukana
jamaa’. Ni mchongo wake kwahiyo hata kama mimi nikibishana ‘nalo’ vipi
kuna mtu mchongo wake yeye anachukua hela.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment