Mkurugenzi wa Habari (MAELEZO), Assah Mwambene amethibitisha jana kuwa
serikali imeyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kwa kile
ilichokiita "kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama." PICHA |
FAILI
Dar es Salaam. Serikali jana ilitangaza kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kuanzia Septemba 27, 2013 kwa kile ilichoeleza kuwa ni mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari za uchochezi na uhasama.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari
(MAELEZO), Assah Mwambene ilisema gazeti la Mwananchi limefungiwa kwa
siku 14 na gazeti la Mtanzania limefungiwa kwa siku 90.
Magazeti hayo yamefungiwa kutokana na kuandika
habari na makala zilizoelezwa zina nia ya kusababisha wananchi wakose
imani kwa vyombo vya dola na kuhatarisha amani.
“Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa
siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba, 2013. Adhabu hii imetangazwa
kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27
septemba,2013,” yasema taarifa hiyo.
Kwa taarifa zaidi, tazama nakala ya tamko
kamili la serikali juu ya kufungiwa kwa magazeti ya Mwananchi na
Mtanzania hapo chini.
TAMKO KAMILI LA SERIKALI
Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya
MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa
magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia
ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo
kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa
siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba, 2013.Adhabu hii imetangazwa
kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27
Septemba, 2013.
Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana
na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na
uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774
ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa
kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka
huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.
Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti,
2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI
YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye
hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi
lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya
kiislam.Jambo ambalo halikuwa la ukweli.
Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo
halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi
linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi
lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari
iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la
Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia
katika maeneo ya ibada. soma zaidi bofya hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment