Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Ndugu wa mfanyabiashara Erasto Msuya (43)aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agosti 7, mwaka huu, wameangua kilio na kuzimia  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, Kilimanjaro baada ya mahakama kuhairisha usikilizaji wa kesi hiyo. 

Ndugu hao  ni dada wa marehemu, Antuja Msuya na Bahati Msuya ambao katika tukio hilo, wote  walipoteza fahamu.

Hali hiyo ilijitokeza baada ya mahakama kuahirisha kesi hiyo kufuatia maelezo ya upande wa mashtaka kuwa upelelezi haujakamilika na hivyo kuzua simazi na majonzi miongoni mwa watu waliohudhuria usikilizaji wa kesi.
 
Wakili wa Serikali Stella
 Majaliwa, aliomba mahakama kuridhia hoja ya kuahirisha shauri hilo ili kutoa nafasi ya kukamilisha shughuli za upelelezi.
 Watuhumiwa walifikishwa mahakamani saa 5: 10, wakiwa ndani ya karandika la polisi.
 Washtakiwa hao ni Sharifu Mohammed (31), mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, na Musa Mangu (38), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu jijini Arusha.
 
Wanatuhumiwa kumuua Msuya kwa kukusudia, kinyume cha kifungu cha sheria namba 196 cha kanuni ya sura 16 ya mwaka 2012. Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Theotimus Swai, aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18 mwaka huu.
 
Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Shaiba Mpunga, hakuwepo mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa ana matatizo ya kiafya.

Mshtakiwa wa kwanza na wa tatu katika kesi hiyo wanatetewa na Wakili Hudson Ndusyepo.


PICHA  ZA  MATUKIO:
 Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya bilionea wa madini Erasto
 Msuya,Sharifu Mohamed na Musa Mangu wakiwa mahakamani.
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha walifurika mahakamani 
kusikiliza kesi hiyo.
 Mtuhumiwa Sharifu Mohamed akiteta jambo na wakili wake 
Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo .
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja
 Msuya baada ya  kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa
 kwa kesi.
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja 
Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya akiangua kilio na baadae kupoteza fahamu mara baada ya 
kuahirishwa kwa kesi.
 Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
 Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
 Mama mzazi wa marehemu Erasto akisindikizwa na wanandugu kwenda kwenye gari la familia.
Umati mkubwa wa wananchi ulifurika mahakamani hapo.
-----Babamzazi.com

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top