Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Muigizaji wa filamu za  kibongo  maarufu  kwa  jina  Jackline Wolper amewaasa waigizaji wenzake wa kike kuacha kuvaa nguo za nusu uchi kwani ni kinyume na mila na tamaduni za kitanzania .

Wolper aliyasema hayo kufuatia kupigiwa kura na kushinda kama muigizaji wa kike mwenye muonekano wa kistaa...


Akizungumza katika kipindi cha filamu cha Take One kinachorushwa Clouds Tv , Wolper alisemakuwa  yeye hawezi kuvaa mavazi ya nusu uchi ila anavaa  mavazi yanayomsitiri mwili wake na bado anapendeza kuliko hao wanaovaa nusu uchi halafu hawapendezi.

"Nawashukuru  sana mashabiki wangu kwa kunipigia kura hadi kuibuka mshindi, na ni kweli najiamini kwa kuwa mimi hata siku moja huwezi kuniona nimevaa nguo za nusu uchi kama wengine" Wolper

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top