Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Raia wa nchini Canada ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya African Barrick Gold Bulyanhulu aliyefahamika kwa jina la Andre Lapierre (50) amefikishwa mahakama  ya mwanzo Lunguya wilayani kahama mkoani shinyanga kwa kosa la kutelekeza mtoto kinyume cha kifungu namba 166 cha sura ya 16 aliyezaa na Bi Elizabeth John.

Akisoma makosa hayo hakimu wa mahakama ya mwanzo Lunguya Derck Masaga ameiambia mahakani hiyo kuwa katika shitaka hilo Andre Lapierre  mwaka jana alimpatia hujauzito Elizabeth john(21) mkazi wa kakola.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa Raia huyo wa Canada  alimpatia ujauzito Elizabeth na kupata mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka moja na nusu sasa na kumuacha bila matumizi.


Kwa upande wake mtuhumiwa huyo  Andre Lapieree alipoulizwa mahakamani hapo  juu ya suala hilo la kutelekeza mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Mariam Andre amesema kuwa siyo kweli kuwa yeye amemtelekeza mtoto huyo.

Akiezea zaidi mahakamani hapo Lapierre amesema yeye hana mashaka na motto huyo hivyo anaiomba  naomba mahakama hiyo , wakapimwe vipimo vya ( DNA) ili ukweli ujulikane.
 


BI ELIZABETH JOHN AMBAYE  AMEZAA NA MZUNGU ANDRE LAPIERRE (50) MFANYAKAZI WA MGODI WA BULHYAHULU AMBAO UNAMILIKIWA NA AFRICAN BARRICK GOLD MINE LTD  AKIWA KATIKA MAHAKAMA YA MWANZO  LUGUYA WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA ALIPOFUNGUA KESI HIYO YA KUTELEKEZWA KWA MTOTO.



Hata hiyo mahakama ilisikiliza hoja hiyo na kutaka kupata upande wa mlalamikaji juu ya suala hilo la kukubali kwenda kwenye vipimo vya( DNA) katika hospital ya serikali na  mkemia mkuu wa serikali na tasisi za serikali  si mahali pengine.

Mahakama ilimuliza Elizabeth kama yupo tayari kwa mtoto wake kupimwa vipimo hivyo naye alisema yuko tayari kwa kuwa hana  wasiwasi kuwa mtoto huyo baba yake ni Endrue.
Mshitakiwa Endrue Lapieree yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili na kutoa shilingi milioni moja.

kesi hiyo  ya jinai yenye namba namba 245/2013, imeharishwa hadi tarehe 4 mwezi wa kumi mwaka huu 2013.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top