Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



white-widow
Wakati mapambano bado yanaendelea dhidi ya wanamgambo wachache wa al Shabaab waliobaki ndani ya Westgate Mall, maofisa wa Kenya wamesema angalau al Shabaab watatu wameuawa katika harakati za kuokoa mateka.


Samantha Lewthwaite, who has been linked with the Kenyon terror attack
Taarifa zinasema mmoja wa magaidi hao ni mwanamke wa kizungu. Inaaminika kuwa mwanamke huyo aliyetajwa ni Samantha Lewthwaite, al-maarufu kama “White Widow” au “Mjane Mweupe” au “Mjane wa Kizungu” kwa Kiswahili. Samantha anaripotiwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo lililofanya mashambulizi.
Inasemekana kwamba kati ya magaidi waliouawa, mmoja wao ni mwanamke wa kizungu lakini bado haijajulikana kama ni Samantha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mume wa Samantha alikua mpiga mabomu wa kujitoa mhanga (suicide bomber) anayeitwa Germaine Lindsay ambaye baada ya kusilimu alitumia jina la Abdullah Shaheed Jamal.

Abdullah Jamal alikua ni mmoja wa magaidi wenye asili ya Uingereza waliopiga mabomu ya kujitoa mhanga katika treni tatu na kuua watu 56 nchini uingereza Julai 7, 2005 ambao unajulikana duniani kama “Ugaidi wa 7/7″
"White Widow" Samantha Lewthwaite na mumewe, 7/7 suicide bomber Germaine na mtoto wao katika picha ya familia
“White Widow” Samantha Lewthwaite na mumewe, 7/7 suicide bomber Germaine na mtoto wao katika picha ya familia
Germaine Lindsay, mume wa "White Widow" wakati wa uhai wake
Germaine Lindsay, mume wa “White Widow” wakati wa uhai wake

Kwa stori kamili ya Samantha na mumewe na picha zao, kama English richabo, nenda kwenye link ifuatayo: Has British 'White Widow' been killed in final assault on Kenyan shopping mall? Body of white woman terrorist is found at scene

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top