Akisimulia tukio hilo kwa mtangazaji wa Radio Times Fm, Edson Mkisi Jr, Binti huyo alisema Babu yake alikuwa akimuingilia mara kwa mara wakati bibi yake akiwa hayupo na kumpa kiasi cha shilingi elfu mbili (2000/=) kama malipo ya alichokifanya na kumsihi asije kumwambia bibi yake.
Taarifa za sasa na zilizothibitishwa na binti mwenyewe pamoja na bibi yake zinadai kwamba, binti huyo kwa sasa ni mjamzito wa miezi mitatu na hakuna mpango wa kuitoa mimba hiyo kwa kuwa si siri tena.
![]() |
| Mtangazaji wa kipindi cha Hatua Tatu ya Times fm, Edson Mkisi Jr (aliyevaa fulana ya njano) akiendelea na mahojiano na Babu. |
Akijibu tuhuma hizo, awali babu huyo aligeuka mbogo na kukanusha tukio hilo na kudai kwamba binti huyo alikuwa na tabia ya kwenda disco na ndipo alipopatia mimba hiyo. Hata hivyo, baada ya kubanwa sana babu huyo alimua kuweka ukweli hadharani na kukiri mimbo hiyo ni yake.
"Kwa kweli ibilisi alinipitia jamani naomba hata kama serikali itanifunga inifunge kifungo cha nje kwa sababu mimi ndio kila kitu pale nyumbani....ni ibilisi tu kwani nililalanae mara moja tu na yeye ndio alinishawishi baada ya kuingia chumbani kwangu wakati ametoka kuoga na mimi kuamua kumpakata na ndio mimba ameingia ingawa sikumuumiza wala kumchana," alijitetea babu huyo mbele ya mkewe kipenzi.
Binti aliyepewa ujauzito na babu
Bibi, Babu na mjukuu aliyepewa ujauzito
Binti akisimulia mkasa
Mashuhuda hawakuwa nyuma kushuhutia tukio hilo.
Aidha, taarifa toka kwa vyanzo vya kuaminika vilidai kwamba babu huyo alishakamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi Mlandizi kwa ajili ya hatua zaidi ya kisheria.
Chanzo:http://mamuafrica.blogspot.com/
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro













Post a Comment
Post a Comment