Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Ammy Nando amesema hana majuto yoyote  baada ya kuondolewa kwenye shindano hilo.

Nando ambaye aliondolewa wiki iliyopita kwa kuvunja  sheria za shindano hilo ,  leo amefunguka  kwa  mara  ya  kwanza ndani  ya  kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“I live my life with no regrets,”alisema Nando  na  kuongeza:

“Sitaki kufikiria  matatizo wala nini, kilichotokea ndio kimetokea...


"Najipanga upya ili  niendelee na maisha mengine. Vingapi vizuri  vimetokea nyuma ? 

"Tokea  nilipokuwa mtoto mdogo nani alikuwa ananijua? Sasa hivi nipo peace , nashukuru kwamba mmenipokea vizuri. 

"Naendelea na maisha, uzuri nimepata platform ya kutengezeza jina langu, kwahiyo naenda hivyo hivyo mpaka huko ntakapofika.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top