
Baada ya kuwa
kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Niwe Nawe Milele, Rehema Chalamila aka Ray C
anatarajia kurejea tena kwa kishindo kwenye muziki. Ray C anatarajia kuonekana
rasmi kwenye shughuli za kawaida na za muziki wiki ijayo. Tumezungumza naye leo
kuhusu maisha yake sasa hivi, alivyobadilika na ujio wake mpya
kimuziki.
Kuhusu kama
yupo tayari kufanya muziki
I am more than
ready, wakati nipo huku nilikuwa naandika andika nina nyimbo kama tatu nne hivi
kali sana. Sema ningependa tu kuwaambia mashabiki wawe na uvumilivu kwasababu
wameniombea sana na wengi kwenye Instagram, Facebook walikuwa ‘when are you
coming back, we miss you’ vitu kama hivyo. Na mimi ningependa kuwaambia tu
kwamba wiki ijayo ndio narudi rasmi, kwa wale ambao walikuwa na wasiwasi, ‘where
is Ray C, Ray C atarudi tena kwenye muziki’ na vitu kama hivyo. Tutaanza kuingia
studio next week, kila kitu kitaanza next week. Lakini kama nyimbo kuandika na
kila kitu vyote viko tayari.
Kuhusu aina
ya nyimbo atakazokuwa akiimba zaidi
Nafikiri sasa
hivi ntabase kwenye maisha zaidi. Nafikiri watu wanahitaji kujua mambo ya maisha
zaidi. Unajua mimi tangu mwanzo nilikuwa naimba mapenzi, ofcourse nyimbo za
mapenzi zitakuwepo sema ntabase zaidi kwenye mambo ya maisha.
Kuhusu
mabadiliko aliyonayo sasa
Ray C ni kibonge
sasa hivi, Ray C amenenepa kidogo. Najua mashabiki wakiangalia kwenye Instagram
wanasema ‘dada vipi bana’ lakini najua njiani huko ntapunguapungua. Lakini Ray C
wa sasa hivi sio kale kembambaa kale mlikokazoea kale. Sasa hivi Ray C kidogo
amevuta shavu kwahiyo wakiniona wasishangae. Halafu pia kwa sauti niko fit sana.
Yaani all along nilikuwa nafanya zaidi mazoezi kwasababu nimepata sana muda wa
kupumzika, mazoezi ya kuimba, yaani nimeona nipo tofauti na
zamani.
Kuhusu sababu
za kunenepa
Si unajua tena
maisha mazuri, kula kula vizuri, kutulia kwa muda bila kufanya kazi ndio maana
nikafutuka kidogo lakini ntafanya mazoezi, ntapungua si unajua lazima nipungue
kidogo ili niweze kuimiliki stage,vile nilivyokuwa zamani au better
zaidi.
Kuhusu
wasanii wapya anaowasikiliza
Namsikiliza sana
ambaye namkubali ni mdogo wangu Recho. I think kwasababu muziki wake kidogo
umefanana na wangu kwahiyo napenda ladha yake halafu kuna Diamond pia
namsikiliza, ni msanii ambaye anafanya vizuri sasa hivi kwahiyo namsikiliza pia
kuna kitu gani hapo watu wanakipendea zaidi niibeibe maideas hapo nifanye kazi
nzuri.
Kuhusu
alivyojiskia baada ya kusikia nyimbo za Recho
Recho mimi
namjua kabla hajatoka na alikuwa anapenda sana nyimbo zangu, alikuwa anasikiliza
sana nyimbo zangu. Mara ya kwanza nimemuona alikuja akaniambia ‘dada Rehema
naomba nikuimbie wimbo mmoja’ akaniimbia ‘Umenikataa Bila Sababu’, akaniimbia
nyimbo kama tatu hivi. Kwahiyo namjua kabla hata hajaingia studio. Kwahiyo
nilikuwa najua kabisa nimemuinfluence kiasi gani.
Tumefurahia
kuona maendeleo mazuri ya Ray C na tunamtakia kila lakheri kwenye safari yake
mpya ya maisha na muziki.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment