IBRAHIM Moses, mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam amenaswa na Polisi wa Kituo cha Mwenge kwa madai ya kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha kanali.
Kanali feki wa JWTZ, Ibrahim Moses baada ya kunaswa na polisi.
Kijana huyo alinaswa na polisi kwa kushirikiana na maafisa wa JWTZ
baada ya kuwekewa mtego kutokana na kudaiwa kuwa alikuwa anajiita Kanali
Ibra, hivyo kutiliwa mashaka hasa baada ya siku moja kuonekana akiwa na
pingu.Habari za kipolisi zinadai kuwa Ibra alikuwa akifika Kituo cha Polisi Mwenge mara kwa mara na alikuwa akipewa heshima zote kama afisa wa jeshi na hasa kwa kuwa alikuwa akitoa ushirikiano wakati wa kunasa wahalifu.
...Akiwa mikononi mwa polisi.
“Alikuwa akija kituoni na kujifanya ni Kanali Ibrahimu akiwa na gari
lake, hivyo kupaki na kupatiwa ulinzi mpaka shughuli zake zinapokwisha
maeneo hayo.“Ilikuwa akikuta watu wamejazana hapa kituoni alikuwa anakuwa mkali na kuhimiza washughulikiwe haraka kwani hapendi kuona watu wamejaa kwenye kituo,” kilisema chanzo chetu kituoni hapo.
...Akipelekwa kituoni.
Chanzo hicho kilidai kuwa walianza kumtilia mashaka baada ya siku
moja kumuachia mfuko wake askari mmoja ambaye alipoudadisi alikuta kuna
pingu, hivyo polisi kuulizana inakuwaje kanali wa jeshi atembee na
pingu.Habari zinasema baada ya hapo mkuu wa kituo hicho cha polisi ilibidi afanye kazi ya ziada kuwasiliana na wanajeshi wa Kambi ya Lugalo ili kujua kama wana afisa wao anayeitwa Kanali Ibrahimu Moses wa Kitengo cha Usalama wa Taifa na Mawasiliano, wakajibu hawakuwa na askari mwenye jina hilo ndipo ulipoandaliwa mtego wa kumnasa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment