H-Baba ameamua kutoa kauli hiyo baada ya kuona watu wanafanya mambo hayo kinyume na Taratibu za Misingi ya Dini,
"Nawapongeza kwa wale wanaoenda kufuturisha watoto Yatima na waendao kufuturisha Misikitini nawapa pongezi sana kwasababu wanapata dhawabu kubwa sana kuliko wale wanaoalika watu wasioeleweka majumbani kwao alfu wanafuturisha alfu usifanye hivyo kutaka sifa unawaita wandishi wa habari nyumbani kwako ili watu wajue, inakuwa siyo swala la msingi.
Lakini uanapokuwa nyumbani kwako ukaalika wasanii wenzako watakuja lakini kumbuka wengine hawajafunga, mwingine katoka bar, Mwingine kasuka, Mwingine kavaa Heleni mwingine kavaa hiki na hiki haiswii kwa sisi watoto wa Kiislamu, Tusitake sifa sisi wasanii tumekuwa wataka sifa.
Leo umesikia Flani kafuturisha eti na wewe kesho yake unaamka na mimi nafuturisha jamani tusifanye kama kamchezo huu ni mwezi wa Ramadhani tuache sifa, Mimi mbona nimefuturisha nani anae jua? kufuturisha ni wewe na ndugu zako na marafikizako wa karibu, siyo leo nafuturisha Mwandishi Flan Njoo unipige picha njoo unimulike Watanzania waone, wewe ndugu yangu mambo hayaendi ivyoo bwana haiswii maana lazima tambiane ukweli unapofanya jambo baya mwezi huu wa ramadhani
Me nimeoa mke wangu ananipikia ftari vizuri nafunga na mpaka kwa sasa kishavu kinatoka,Nafuturisha watu wanakuja kwangu wanafuturu lakini siyo kwa sifa sasa mnaita mpka TV, Magazeti na Redio aaah jamani nani wewe? sifa za nini kipindi hiki ? unatubu nini sasa? jamani wasanii wenzangu nawasii tuache sifa namaliza kwa kusema KWA ALLAH HAKUNA SIFA" alisema H-BABA
ANGALIA VIDEO CHINI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment