Kama ule usemi usemao hatujui
yatakayo tokea kesho, ndicho kilichotoa muda mfupi uliopita majira ya
saa moja jioni jana tarehe 02/07/2013, baada ya gari dogo lililokuwa
linatokea maeneo ya Ubungo kwenda uelekeo wa Buguruni kumgonga mwenda
kwa miguu aliyekuwa anavuka barabara katika maeneo gereji (garage)
Maeneo haya ni mara baada ya kituo cha daladala mabibo external, kituo
kinachofuata kama unakwenda Buguruni kinaitwa gereji, hapa ndipo
ilipotokea ajali hiyo
Mtu aliyegongwa hakuweza kufahamika
kwa wakati huo na mashuhuda wengi wa ajali hiyo, lakini ni kijana wa
kiume mwenye umri kati ya miaka 30 na 22, rangi yake ni mweusi, na
alikuwa amevaa t-shirt nyeupe iliyokuwa na maandishi ya ADIDAS,
Kwa hakika maisha yetu wanadamu ni
mafupi sana!! tunaweza kuwa na mipango mengi na malengo mazuri sana,
lakini mwisho wetu ukawa hivi pasipo hata kutarajia!! ndio maana wale
wanao amini juu ya maisha mengine baada ya kifo, wanafundisha na kusema
tunapaswa kujiweka tayari kiroho wakati wote
Damu ilimtoka kwa wingi sana mara
baada ya ajali katika maeneo ya kichwani, na hapo ilipotokea ajali kuna
kivuko cha waendeo kwa miguu!! kwa mtazamo usio na uthibitisho wa
daktari, kijana huyo alifariki muda mfupi baada ya ajali. Tunaomba
kuchukua nafasi hii kuwakumbusha madereva wote wazingatie sheria za
usalama barabarani, hapa ilipotokea ajali kuna kivuko cha waenda kwa
miguu na pia kuna kituo cha mabasi (daladala) kwa vyovyote dereva
alitakiwa kupungumza mwendo na hata kama pa mtu anavuka angeweza kumwona
na kuepusha ajali. Tunaliomba jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani, wasichoke kuwaelimisha madereva juu ya alama za barabarani
chanzo:http://darubinileo.blogspot.com/
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment