Kwa mujibu wa
wananchi waishio maeneo hayo, wamekuwa wakikerwa na vitendo vya kifuska
vinavyofanyika katika nyumba hiyo inayodaiwa kumilikiwa na mwanamke aliyefahamika kwa jina la Deograsia Nchimbi.
Baada ya wananchi hao kutoa malalamiko kwa mama huyo mara
kwa mara bila mafanikio, waliamua kukitaarifu kikosi kazi cha waandishi
wa Global Publishers Ltd ili waweze kufanya kazi yao.
“Kwa kweli tumesema hadi tumechoka huyu mama amekuwa chanzo cha kuharibu tabia vijana wetu, nyumba yake imekuwa kero, tunaomba Global mfanye kazi
yenu ya kufichua maovu.
“Ngono
zembe zinafanyika waziwazi bila hata ya kificho, hata sijui tunakipeleka
wapi hiki kizazi cha sasa!” alisema mkazi wa eneo hilo aliyeomba
hifadhi ya jina.NA GPL
OFM KAZINI
Baada ya kupokea taarifa hizo, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua
Maovu (OFM) inayoendeshwa na Kampuni ya Global, kiliingia mzigoni na
kufanya uchunguzi, kilipobaini ukweli ndipo kilipolitaarifu Jeshi la
Polisi, Buguruni kisha kuvamia.
Kikosi kazi cha OFM na polisi walivamia katika nyumba hiyo hivi
karibuni majira ya saa kumi na mbili jioni na kuwakuta vijana hao wakiwa
na bangi lakini mama mwenye nyumba hakukutwa na kidhibiti.
Ndani ya nyumba hiyo walikutana na vijana wasiopungua
kumi lakini waliposikia mlango unafunguliwa walitimka na kuiacha
misokoto ya bangi sebuleni ambapo polisi walifanikiwa kumkamata Amosi
Nchimbi aliyedaiwa kuwa ni mtoto wa mama mwenye nyumba pamoja na
wasichana wawili.
WAFIKISHWA POLISI
Baada ya purukushani ya hali ya juu kati ya polisi na vijana hao
waliodaiwa kugeuza nyumba hiyo kuwa danguro, walifanikiwa kuwatia
mbaroni wasichana wawili na mtoto huyo wa mwenye nyumba ambapo hadi OFM
inaondoka eneo hilo, iliwaacha polisi wakiwa katika harakati za
kuwapeleka watuhumiwa Kituo cha Polisi cha Buguruni.
WANANCHI WACHEKELEA
Wananchi pamoja na diwani wa mtaa huo, Mtumwa Mohamed walifurahi
kuona vijana hao wakipelekwa polisi kwani hali hiyo ilikuwa ikiharibu
tabia za vijana wao kwa muda mrefu hivyo kuishukuru OFM kwa jitihada
zake za kufichua maovu katika jamii.
“Nawashukuru kwa kweli hapa palikuwa ni kama chaka la maovu nadhani
sasa hali hii itatulia. Hili eneo lilikuwa linaleta picha mbaya kabisa
katika jamii,” alisema Mtumwa.
SOURCE: GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment