Washindi wa pili wa ligi kuu ya England kwa msimu uliopita Manchester
City wameendelea kufanya usajili wa kuimarisha kikosi chake baada ya
kuwa kwenye harakati za mwisho za kusajili striker wa kimataifa toka
Montenegro Stevan Jovetic .
Mchezaji huyo alionekana akiingia kwenye hoteli moja huko Manchester akitokea Italia tayari kukamilisha usajili wake toka Fiorentina . Jovetic mwenye umri wa miaka 23 anasajiliwa kwa paundi milioni 25.8 ambapo Coty watalipa paundi milioni 22.4 za awali kabla ya kumalizia nyingine kuendana na aina ya mchango toka kwa mchezaji mwenyewe na mafanikio ambayo City itayapata katika kipindi cha mkataba wake .
Usajili huu unaokaribia kuliziwa siku chache zijazo unakuja zikiwa zimepita saa 24 tangu City ilipofanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Hispania Alvaro Negredo na kufanya idadi ya wachezaji waliosajiliwa kufikia wachezaji wanne baada ya usajili wa Fernandinho na Jesus Navas huku jumla ya paundi milioni 87 zikiwa zimetumika kwa wachezaji wote .
Navas alisajiliwa kwa paundi milioni 15 , Fernandinho kwa paundi milioni 30 , Alvaro Negredo paundi milioni 20.6 na Jovetic paundi milioni 26.
Ujio wa Negredo na Jovetic utamlazimu wakala wa mshambuliaji toka Bosnia Edin Dzeko kuingia kazini kusaka timu ya mteja wake kucheza endapo atataka kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha wachezaji 11 wanaoanza kwenye kila mechi kwani nafasi yake ndani ya Kikosi cha City inazidi kuwa finyu.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment