Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

clip_image002Snura Mushi mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI wa kike na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi amedai kuwa muziki ulimpa dili ya kwenda kurekodi filamu Afrika ya Kusini, anasema kuwa watayarishaji wa filamu ya Tandeka iliyorekodi jijini Pretoria kwa kuwashirikisha wasanii watanzania waishio Afrika ya Kusini imetokana na kufanya vizuri katika muziki hasa
nyimbo yake ya Majanga.
clip_image002[8]Snura Mushi akiwa katika pozi matata.
Filamu kwa sasa inachangamoto sana hilo lilinifanya nirudi katika muziki huku nikichagua filamu za kuigiza na kujikita katika muziki zaidi ambao unanifanya niwe bussy sana, lakini ninachofurahia kupitia nyimbo yangu ya majanga nilipoenda kuirekodia Afrika kusini pia nilipewa uhusika mkuu kuigiza filamu ya Tandeka,”anasema Snura.
clip_image002[10]Snura anadai kuwa watayarishaji walimuona na kumwita katika usahili aliposhinda alipewa muswada (Script) na kuigiza kama mhusika mkuu ambaye aliigiza kwa umahiri mkubwa filamu ya Tandeka imetumia lugha mbalimbali ikiwa Kiswahili, Kizulu na Kiingereza, Snura ni msanii mwigizaji wa filamu aliyetokea katika tamthilia ya Jumba la Dhahabu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top