MAANDAMAANO ya makundi hasimu yalifanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo na katika maeneo mengine kote nchini humo Jumapili, pale wafuasi na wapinzani wa Rais aliyeng’olewa madarakani Mohammed Morsi walipomiminika mitaani kutetea misimamo yao ya kisiasa. (HM)
Nao wapinzani wa Morsi pia wakipanga kufanya maandaamano yao katika Tahrir Square.
Na huku maandamano ya kuunga na kumpinga rais Morsi yakiendelea, kaimu rais wa Misri Adly Mansour, anaendelea kujadiliana na viongozi wa upinzani juu ya kuunda serikali mpya.
Taarifa za Jumamosi kwamba kiongozi wa upinzani Mohammed ElBaradei amechaguliwa kuongoza serikali kama waziri mkuu, zilikanushwa na msemaji wa rais Ahmed Al Muslimany.
Alisema majadiliano yameanza lakini jina la waziri mkuu mpya bado halijaafikiwa. Alisema Mohammed el Baradei ana nafasi nzuri zaidi kuchukuwa wadhifa huo lakini maamuzi rasmi bado hayajatolewa kwa vile mazungumzo ya kisiasa bado yanaendelea.
Wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood na wale wa chama cha Salafi Nour party, wanapinga uteuzi wa ElBaradei.
Viongozi wa Muslim Brotherhood wanasisitiza hawatashiriki katika utaratibu wowote wa mpito hadi pale rais wa zamani Morsi atakaporejeshwa madarakani. Nao wanamgambo walilipua bomba kuu la mafuta huko kaskazini mwa Sinai Jumapili na kusababisha moto mkubwa.
Bomba hilo linalopeleka mafuta kwa nchi jirani ya Jordan, limeshambuliwa mara kadha tangu kupinduliwa kwa rais Hosni Mubarak hapo February mwaka 2011.Chanzo: voaswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment