Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Elizabeth michael (Lulu) asisitiza kuwa lazima atarudi shule kusoma hivi karibuni.
Mwanadada wa bongo movies Elizabeth Michael maarufu kama Lulu  amekazia nia yake ya kutaka kurudi shule siku chache zijazo.
Katika kipindi cha kikaangoni live cha East Africa Television mwanadada huyo aliulizwa swali na mmoja wa mashabiki wake kama ana mpango wowote wa kurudi shule hivi karibuni.Elizabeth michael (Lulu) asisitiza kuwa lazima atarudi shule kusoma hivi karibuni. 1
Lulu alijibu kwa kusema  kuwa yupo kwenye mchakato huo wa kurudi kumalizia elimu yake ya sekondari aliyoikatisha.
“Am on process..soon mpenzi nitarudi darasani,” aliandika Lulu ambaye awali alidaiwa kukatisha masomo yake ya sekondari kutokana na kujiingiza kwenye fani ya uigizaji.
Mwanadada huyu anatarajiwa kutoa Filamu yake mpya na ya kwanza ya foolish Age inayotarajiwa kutoka mwezi ujao.
                         chanzo bongomovies

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top