Kwa heri ; Tito Vilanova akizungumza na wachezaji wake katika mazoezi ya jana
Huzuni kubwa: Sandro Rosell na Andoni Zubizarreta wamethibitisha kuondoka kwa kwa Vilanova
Rais
wa Barca, Sandro Rosell na Mkurugenzi wa Michezo, Andoni Zubizarreta
wamethibitisha kubwaga manyanga kwa Vilanova katika mkutano uliofanyika
usiku huu.
Msaidizi
wa Vilanova, kocha wa zamani wa Girona, Joan Francesc Ferrer ‘Rubi’,
anatarajiwa kuteuliwa kocha wa muda wa dharula, wakati klabu ikitafuta
kocha wa kudumu.
Kazi ngumu sana: Rosell atatafuta mrithi wa Vilanova
Daah! baba anasepa: Mchezaji muhimu wa Barca Lionel Messi anaweza kuathiriwa sana kuondoka kwa kocha wake
Afya mgogoro: Vilanova ameachia ngazi kuinoa Barca ili akatibu matatizo yake ya saratani
Haya sasa kazi kwako: Joan Francesc Ferrer anakabidhiwa matunguli ya Tito
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Rais
wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell, amethibitisha kuwa Tito Vilanova
amebwaga manyanga kuifundisha klabu hiyo kutokana na matatizo ya kiafya
yanayomkabili kwa sasa.
Vilanova
mwenye umri wa miaka 44, aliyerithi mikoba ya Pep Guardiola msimu
uliopita amelazimika kujiuzulu kufuatia kuendelea kwa tatizo lake la
saratani na mpaka sasa anajiandaa kwenda kupata matibabu nchini Marekani
baada ya tatizo lake kujirudia tena.
Barcelona kupitia mtandao wao wa kiofisi wamesema: ’Tito Vilanova hataendelea kuwepo katika benchi la Barca”.
Rais Sandro Rosell ametangaza ijumaa ya leo kwamba kocha huyo wa wazee wa Katalunya hataweza kufundisha msimu ujao
Katika
mkutano mfupi ambao viongozi wa bodi ya klabu ya Barcelona walikutana,
Rosell alisema: “Habari nilizonazo ni zile ambazo hamtapenda kupokea”.
“Kufuatia kutathimini ratiba ya matibabu ya Tito, sasa mambo yamekuwa magumu zaidi, hataweza kuwa kocha mkuu”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment