Isabela Mpanda ‘Bela’ na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
Kina dada wanaounda Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda ‘Bela’ na
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ wametofautiana hadi kufi kia hatua ya
kutukanana na kutupiana nguo nje.
Mpango mzima ulitokea hivi
karibuni Kijitonyama jijini Dar, nyumbani kwa Isabela ambapo chanzo cha
ugomvi huo ni baada ya Isabela kumsifia mtandaoni X-memba wa kundi lao,
Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ kwa kununua gari, ndipo Kabula
alipokasirika na kuanza kumtukana Bela na mama yake matusi ya nguoni.
“Sikumuelewa
kabisa Jini, kumsifi a Jack kuhusu kumiliki gari ndiyo kumemfanya
anitukane? Iliniuma sana na sitamsamehe, bora kila mtu achukue hamsini
zake, nguo zake nilimtupia nje,” alisema Bela na kusisitiza kufanya
muziki peke yake kwa sasa.
Alipotafutwa Jini Kabula kuhusiana na
sakata hilo, simu yake iliita bila kupokelewa achilia mbali kujibu
ujumbe wa BBM ambao alitumiwa na mwandishi wetu
Post a Comment
Post a Comment