ARSENAL jana usiku walivunja rekodi yao ya usajili baada ya kukubaliana na Madrid kulipa kiasi cha £23million kwa ajili ya kumsaini Gonzalo Higuain.
Muargentina huyo atafanyiwa vipimo na Gunners leo na anategemewa kusaini mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya100,000 kwa wiki.
Higuain, 25, amepewa ruhusa na Madrid kusafiri kwenda London baada ya mazungumzo marefu yaliyodumu kwa wiki kadhaa.
Dili hili ambalo limethibitishwa na baba yake Higuain linakuja kuleta nafuu kwa mashabiki wa Arsenal waliokuwa wakililia kocha wao asajili wachezaji wa daraja la dunia, ili kuweza kukata kiu ya zaidi ya miaka nane ya kutwaa kombe.
Santiago Cazorla ndio alikuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Arsenal – akiwa amesajiliwa kwa zaidi ya paundi millioni 16 akitokea Malaga.
Golikipa Julio Ceasar ndio anatajwa kumfuatia Higuain kwenda Emirates akitokea QPR ambao wameshuka daraja.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment