Hatimaye
mwadadada Wastara Sajuki amerejea tena kwenye ulimwengu wa filamu baada
ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye tasnia hii kutokana na matatizo
aliyoyapata ya kuondokewa na mumewe Juma Kilowoko (Sajuki) mnamo mwezi
wa January mwaka huu.
Akizungumza
katika utengenezaji wa Filamu yake mpya ya kwanza atakayoiachia wastara
amesema Filamu hii mpya wastara amesema kuwa itahusu maisha ya kawaida
ya mwanadamu na jinsi ambavyo matatizo yanayomkabili binadamu
yanavyoweza na kumuathiri kisaikolojia na kumpelekea kufanya mambo
ambayo hakuwai kuyafikiria.
Wastara
amesema kisa kikuu kwenye filamu hii yake mpya ni jinsi familia moja
iliyokuwa na maisha mazuri na baadaye mama wa familia kupata kansa ya
kizazi na kupelekea kuondelewa kizazi chake kabla ya kufiwa na mtoto
wake pekee aliyekuwa naye na namna ambayo mumewe anavyojaribu kumliwaza
mkewe kwa matatizo hayo yanayotokea.
Wastara
amesema kuwa kwenye Filamu hii ameshirikia na waigizaji Yusuph Mlela na
Nisha pamoja na mwigizaji mweingine aliyemtaja kwa jina la Hamida na
amewataka wapenzi wake wote wakae mkao wa kula kwa ajili ya Filamu hii
inayotarajiwa kutoka mwezi wa tisa.CHANZO BONGO MOVIE
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment