Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na
wengine wengi kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka
kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni
jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika
maeneo ya jiji hilo.
Waliojeruhiwa
wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi
ya watu waliojitolea wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa
hospitali hizo kutoa huduma ya kwanza.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo.
Bomu
hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka
mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa
umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.
Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA. Mwandishi mmoja wa habari anaripotiwa kunyang’anywa kamera yake baada kwa kupiga picha, hata baada ya kujitambulisha.
Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.
Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Seliani na Mount Meru.
Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.
Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA.
ILANI: Baadhi ya picha zilizopachikwa hapo huenda zikagusa hisia ya mtizamaji, tafadhali ikiwa huwezi kuvumilia kuona damu usibofye tarakimu zilizopo hapo chini kufungua picha zinazofuatia.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro