Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Injini ya ndege hiyo ikiwaka moto wakati ikiwakwenye harakati za kuruka.
Hili ni tukio la kushangaza pale moja ya injini za ndege iliyobeba zaidi ya abiria 300 ilipolipuka wakati ikijiandaa kuruka.


Ndege hiyo Airbus A330 alikuwa ikiambaa kwenye njia ya kuruka/kutua katika Uwanja wa Ndege wa Manchester juzi ndipo injini yake ya upande wa kulia ghafla ikapata hitilafu na kulipuka.
Ndege hiyo kwa bahati ilikuwa bado haijaruka na rubani huyo aliweza kwa haraka kuidhibiti.
Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Thomas Cook namba TCX314 ilikuwa imebeba abiria 325 kuelekea Jamhuri ya Dominika wakati wa tukio hilo.
Picha ya kushangaza ya video iliyorushwa kwenye mtandao inaonesha jinsi injini hiyo ghafla ikilipuka wakati ndege hiyo ikichukua kasi kwenye njia yake.
Huduma za dharura yakiwamo magari matatu ya zimamoto kisha yakawasili eneo la tukio kukabiliana na hatari yoyote ambayo ingeweza kutokea.
Msemaji wa Shirika la Ndege la Thomas Cook alithibitisha uchunguzi ulikuwa unatarajiwa kuanza wakati wowote kuhusiana na tukio hilo.
Msemaji huyo alisema: "Tunathibitisha kwamba tukio hilo limetokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Manchester na kuhusisha ndege TCX314, wakati ikiruka kuelekea Jamhuri ya Dominika.
"Ndege hiyo ilipata hitilafu kwenye injini na kurejea kwenye maegesho; kama tahadhari, huduma za dharura uwanjani hapo wakaishughulikia ndege hiyo - lakini mpaka wakati huyo hakuna abiria yeyote au wafanyakazi waliopata madhara.
"Tunapenda kuwashukuru wateja wetu kwa uvumilivu wao wakati wote wa kuchelewa kwa ndege yao; ndege mbadala ilitumika kuwabeba kuelekea kwenye mapumziko yao mchana huo huo."

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top