Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
KAMANDA SULEIMAN KOVA
Baada ya jana mtandao huu wa thesuperstatz kuripoti juu ya msichana mrembo kukutwa jalalani akiwa amechinjwa na watu wasiojulika .kwasasa jeshi la polisi limeanza kupata mwanga mara baada ya kumshikilia philemon Laiza ambaye amekiri kuhusika na tukio hilo  hii hapa ni taarifa kamili.

MFANYAKAZI wa Jaji Kileo, Philemon Laiza (27) anadaiwa kumchinja mtumishi wa ndani wa jaji huyo, ambaye ni raia wa Kenya, Perpetua Mainab (30). Mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa ni mtunza bustani katika nyumba ya Jaji Kileo, alifanya unyama huo wiki iliyopita. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema mwili wa mtumishi huyo wa ndani ulikutwa kwenye dampo la kutupia takataka maeneo ya Mikocheni B.

“Tukio hilo lilitokea karibu na dampo la kutupia taka Mikocheni ‘B’, katika eneo linalomilikiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

“Mfanyakazi huyo wa ndani alikutwa ameshakufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo, jeraha sehemu ya mkono wa kushoto karibu na kiganja, jeraha kwenye paji la uso na mwili wake ukiwa umetapakaa damu sehemu za kichwani,” alisema Kova.

Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja na marehemu, alikiri kuwa na marehemu siku hiyo ya Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu.

Alisema baada ya polisi kufanya upelelezi mtuhumiwa alikutwa na kiatu kimoja cha marehemu na nguo alizovaa siku ya tukio, ambazo zilikuwa zimetapakaa damu.
MWILI WA MAREHEMU PEPETUA ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA JAJI KILEO UKIWA UMETUPWA JALALANI KAMA TAKA MARA BAADA YA KUCHINJWA KAMA KUKU

“Nguo hizo za marehemu zilikuwa zimetapakaa damu na baada ya mahojiano ya muda mrefu, mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo.
Kamishna Kova alisema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alidai kuwa marehemu alitoweka nyumbani tangu siku ya Ijumaa na baada ya kubanwa na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo.

Kova alisema mtuhumiwa bado anahojiwa na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Katika tukio jingine, jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata majambazi nane wanaojihusisha na uporaji mali za raia wa kigeni katika fukwe ya Bahari ya Hindi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top