Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
KLABU ya Liverpool imetangaza kumsaini mshambuliaji wa Sevilla, Luis Alberto kwa dau la Pauni Milioni 6.8.
Mspanyola huyo mwenye umri wa miaka 20, amesaini mkataba wa miaka minne na Wekundu hao.
Akiwa ametumia msimu uliopita kucheza kwa mkopo Barcelona B, Alberto amefunga mabao 11 na kutoa pasi safi 17 za mabao katika mechi 38 katika kikosi hicho cha wachezaji wa akiba wa timu hiyo ya Catalan.

Amesajiliwa: Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Luis Alberto

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema katika mtovuti ya klabu hiyo: "Tuna furaha kwamba Luis ameamua kujiunga na Liverpool. Ni mchezaji mwenye sifa za na uwezo wa kuichezea Liverpool.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top