Mhadhiri
wa chuo kikuu cha Delta State huko nchini Nigeria alijikuta katika aibu
kubwa baada ya kuvuliwa nguo na kubaki uchi wa mnyama baada ya
mwanafunzi wa kike aliyekuwa akisumbuliwa na Mhadhiri huyo kuamua
kumfanyia umafia kwa kumuwekea mtego.
Hatua ya kudharirishwa kwa Mhadhiri huyo ilikuja baada ya
mwalimu huyo kumtishia Tega na kumwambia kuwa atamferisha kama hata
kubali kufanyanae mapenzi.Kabla ya hapo Mhadhiri huyo aliwahi kumtongoza
mwanafunzi huyo lakini mwanafunzi huyo alimkatalia kata kata baada ya
kuona hivyo Mhadhiri huyo aliamua kutumia wadhifa alionao kwa kumtishia
kuwa kama hato kubali kulala nae basi atamfelisha mtihani.
Baada ya kuona hivyo Tega aliamua kumkubalia Mhadhiri huyo na
kumshawishi badala kwenda kwenye hoteli kuchukua chumba ni bora waende
nyumbani alikopanga mwanafunzi huyo ili wapunguze gharama,kuona hivyo
Mhadhiri huyo alikubali haraka na kwenda nyumbani kwa Tega bila kujua
kuwa kuna mtego amewekewa kumbe kabla ya hapo Tega alikuwa amesha
waambia majirani zake na wanafunzi wenzake kuwa atahakikisha anamrubuni
Mhadhiri huyo mpaka akubali kuvua nguo akisha kubali tu anamuaga kuwa
anakwenda chooni kisha anawapigia simu waje kumuumbua Mhadhiri huyo
kwani milango yote alikuwa ameirudishia tu na alikuwa ameshawaelekeza
chumba ambacho atakuwepo Mhadhiri huyo.
Basi baada ya kuwapigia majirani na wanafunzi wenzake walifika eneo hilo la tukio na kufungua milango kimya kimya na kufanikiwa kuingia ndani mpaka chumba alipo Mhadhiri huyo ndipo walipo fanikiwa kumkuta Mhadhiri huyo akiwa uchi wa mnyama kitandani na kisha kumtoa nnje na kumtembeza uraiani ili watu wajionee wenyewe nini baadhi ya wahadhiri hufanya kwa wanafunzi wa kike.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment