Washirika wa Somalia Afrika Mashariki nzima na Mashariki ya Kati
wanajitolea kusaidia kujenga upya taasisi za jeshi la Somalia kupitia
msaada wa kifedha na kiufundi.
Wanajeshi wa Jeshi la Taifa la Somalia
wakitembea wakati wa gwaride la kijeshi karibu na sehemu iliyokarabatiwa
ya Wizara ya Ulinzi huko Mogadishu. Misri imeomba kumalizia ujenzi wa
jengo. [Stuart Price/AU-UN IST/AFP]
Misri ni nchi ya kanda ya hivi karibuni ambayo imeahidi kusaidia kujenga upya miundombinu ya jeshi la Somalia, ambayo iliharibiwa na miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Misri ni nchi ya kanda ya hivi karibuni ambayo imeahidi kusaidia kujenga upya miundombinu ya jeshi la Somalia, ambayo iliharibiwa na miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
"Serikali mpya ya Somalia imedhamiria kukarabati majengo ya jeshi na
kuvijenga upya vikosi vya jeshi … kwa kutumia misingi ya kisasa na ya
hali ya juu na kwa msaada wa nchi rafiki, ikiwemo Misri, ambayo
kihistoria imechangia katika kuvisaidia vikosi vya jeshi vya Somalia,"
alisema Admiral Farah Qare, kamanda wa vikosi vya majini vya Somalia.
Qare aliongoza kamati ya serikali ambayo ilipokea ujumbe wa ngazi ya juu
kutoka Jeshi la Ulinzi la Misri tarehe 4 Juni huko Mogadishu.
"Majengo ambayo Wamisri wanadhamiria kusaidia kujenga upya ni makambi
kadhaa ya jeshi na hospitali katika makao makuu na ofisi za Wizara ya
Ulinzi ya Somalia," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba mchakato ungeanza
katika miezi michache inayokuja.
Kanali mtsaafu Mohamed Ali Moalim, aliyefanya kazi katika jeshi la taifa
la Somalia chini ya aliyekuwa Rais Mohamed Siad Barre, alisema vikwazo
vya silaha vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Somalia kilikuwa kizuizi kwa
serikali na kuzuia msaada uliotakiwa kuendeleza jeshi la taifa
linalofaa.
"Uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kupunguza vikwazo
vya silaha kwa Somalia kwa mwaka mmoja umezihamasisha nchi rafiki na
zile zinazojali suala la Somalia kuisaidia serikali ya Somalia katika
jitihada zake za kujenga upya jeshi la taifa," Moalim aliiambia Sabahi.
Jeshi la Somalia linahitaji kufanya uchunguzi kamili ili kutimiza majukumu yake kikamilifu, Moalim alisema.
"Ili kuunda jeshi imara lenye uwezo wa kufanya kazi zake za usalama na
kupanua udhibiti wa serikali nchi nzima, ni muhimu kuanzisha amani
nchini Somalia," alisema. "Viongozi wapya wanahangaikia kuunda jeshi
imara la taifa katika nyongeza ya kufanya kazi kuelekea kuwahusisha
wanachama wa wanamgambo wenye silaha ndani ya vyeo vya jeshi la
kawaida."
Wizara ya Ulinzi ilieleza kuanza kazi ngumu ya kuliunda upya jeshi mwezi
Februari pamoja na uhamishaji wa makazi yasiyo rasmi na watu wasiokuwa
na makazi ndani ya nchi kutoka katika nyumba za jeshi na hospitali.
"Wizara ya Ulinzi Somalia imefanikiwa kuhamisha taasisi kadhaa za jeshi,
ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege kando ya Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mogadishu, kituo cha burudani cha maofisa cha Circolo
Ufficiale katika wilaya ya Howlwadag na hospitali ya jeshi huko Hodan,"
alisema Ahmed Hussein, kaimu msaidizi wa miundombinu katika Wizara ya
Ulinzi.
Misri, Uturuki, Sudani na Djibouti zimeahidi kuchangia ukarabati wa
taasisi za jeshi, alisema Hussein, ambaye pia yupo katika kamati ambayo
inasimamia uhamishaji wa mali za jeshi.
Naibu Waziri wa Kazi za Umma na Ujenzi Mpya Nadifo Mohamed Osman alisema
kumekuwa na matakwa mapya ya nchi ya Uarabuni kuisaidia Somalia.
"Misri, Iraki, Saudi Arabia, Djibouti, Sudani, Jamuhuri ya Falme za
Kiarabu, Kuwait na nchi nyingine zimejituma kwa kiasi kikubwa, kama vile
kufadhili mradi wa ujenzi mpya nchini Somalia na kuwafundisha wanajeshi
wa Somalia kama sehemu ya muundo wa jitihada za kusaidia serikali mpya
ya Somalia," aliiambia Sabahi.
Wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za shirikisho Uarabuni, nchi
wanachama zilikubaliana kuisaidia Somalia katika siasa, fedha na ufundi
kusaidia serikali mpya kuendeleza siasa, kuhamasisha usalama na kusaidia
jitihada za ujenzi mpya.
"Iraki imeahidi Dola milioni 15 kutekeleza mradi kadhaa ya ujenzi nchini
Somalia ambayo inahusisha ukarabati wa taasisi mbalimbali za serikali
na makao makuu ya Wizara ya Kazi za Umma na Ujenzi mpya, pamoja na
taasisi za mafunzo na hospitali ya wagonjwa wa akili huko Mogadishu,"
alisema Osman.
Chanzo: sabahionline.com
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment