STAA anayeng’aa katika Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
amemsuta mganga aliyejitokeza na kudai kwamba mwaka huu staa huyo
hatapata mafanikio yoyote na atapotea katika fani.
Mganga huyo ambaye alidai utaalamu wake ndiyo uliompandisha chati
Diamond alisema mwaka huu staa huyo hatapata tuzo, atafifia na jina
lake litasahaulika kutokana na kukiuka masharti yake. Akizungumza na
Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisisitiza kutomtambua mganga huyo na
anamshangaa kwa kuwa mwaka huu amepata mafanikio tofauti na alivyosema. “Hebu
angalieni, mganga alidai mwaka huu nitafutika katika fani, mbona
nimepata tuzo mbili kwenye Kil na nimechaguliwa kuwa balozi wa Cocacola
na shoo zinajaza kinoma?” alihoji Diamond. Aidha, alisema shoo zake
bado zinajaza watu wengi huku akiitolea mfano ya mwisho iliyofanyika Dar
Live, Mbagala Zakhem, Dar hivi karibuni iliyojaza nyomi ya watu.
source talkbongo
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment