Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mmoja wa shabiki wa marehemu Albert Mangwea aliyeanguka na kupoteza fahamu wakati kuuaga mwili wa msanii huyo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.Picha na Habarimpya.com
WATU sita wameanguka na kupoteza fahamu wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa Kizazi kipya nchini Tanzania katika viwanja vya Leaders Club, watu hao ni wanawake wanne na wanaume wawili na wanaendelea kupewa huduma ya kwanza kutoka kwa kikosi cha msalaba mwekundu waliopo katika viwanja hivi na kuwapa huduma ya kwanza.
Mwandishi wa Habarimpya.com akiwa katika viwanja hivyo jijini Dar es Salaam anasema kwamba umati mkubwa umezidi kuongezeka katika viwanja hivyo huku vilio vikitawala.
Wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya wakiongozwa na msanii maarufu Abdul Nassib (Diamond Platinumz) wamejitokeza kwa wingi katika tukio hilo kihistoria katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Akizungumza na Habarimpya.com katika viwanja hivyo msanii aliyewahi kutamba na kibao chake cha kwanza cha Zeze langu T.I.D ambaye kwa sasa anatamba na Bendi yake ya muziki ya Top Band amesema kwamba, "Kuna mipango mingi tulipanga na Mangwea lakini leo nasikitika sana kuona nimebaki peke yangu".

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top