

Nayman akimtoka beki wa Mexico


Shabiki wa Brazil

Brazil imeilaza Mexico mabao 2-0 bila ubishi na sasa inatimiza ponti sita na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa Kundi A.
Daniel Alves alipinda krosi kutoka kulia na nyota mpya wa Barcelona, Neymar akaitokea wa kwanza mbele ya beki wa Mexico, kabla ya kuhadaa na kumtungua kipa Jose Corona dakika ya tisa na dakika ya 90 akampa pande Jo kufunga la pili.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Howard Webb wa Uingereza, kikosi cha Brazil kilikuwa: Cesar, Alves, Silva, Luiz, Marcelo, Luiz Gustavo, Paulinho, Oscar/Hernanes dk62, Hulk/Lucas Moura dk78, Neymar na Fred.
Mexico: Corona, Rodriguez, Salcido, Torrado, Dos Santos, Henandez, Moreno, Guardado, Torres/Barrera dk70, Mier na Flores/Herrera dk68.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro









Post a Comment
Post a Comment