Shuhuda
wetu ambaye ni dereva wa bodaboda aliyefahamika kwa jina la Shabani,
alisema tukio hilo lilitokea Juni 11, mwaka huu maeneo ya Mafiga karibu
na Msikiti wa Mahita ambapo Khadija alichukua uamuzi huo baada ya
mwanaume aliyezaa naye kumgomea mtoto kwa madai ana nywele za Kiarabu
hivyo si wake.
“Huyu dada alifika kwenye kijiwe chetu akiwa amembeba mtoto mgongoni na kukodi pikipiki ili nimpeleke mjini.
“Tulipofika kwenye msitu uliopo karibu na mashamba ya SUA, aliniambia niendeshe spidi kuna mtu anamuwahi.
Nilitii amri lakini tulipofika mbele kidogo nikashangaa anamtupa yule mtoto.
“Nilipoona
vile nilisimama na kumhoji kwa nini anafanya vile, akawa hajibu.
Nikamchukua na kumpeleka kituo kikuu cha polisi akiwa hana mtoto. Baadae
wasamaria wema walimuokota mtoto akiwa ameumia na kumfikisha polisi,”
alisema mtoa habari huyo.
Mwandishi
wetu alifika katika kituo hicho cha polisi na kufanikiwa kumkuta
Khadija akiwa chini ya ulinzi mkali huku mwanaye akitokwa na damu usoni
na alipoulizwa kulikoni alisema:
“Jamani
naomba msamaha, nimefanya hivyo kwa hasira baada ya baba wa mtoto kudai
si wake, eti ni Mwarabu wakati yeye ni Mngoni wa Songea, nisameheni
sitarudia tena.”
Akizungumza
na mwandishi wetu, Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Morogoro, Tausi
Mbalamwezi alisema mwanamke huyo amefanya kitendo kibaya na sasa
wanamsaka baba wa mtoto ili amlee huku mtuhumiwa akisuburi taratibu
nyingine.
“Yupo
hapa na tumemkuta na kadi ya kliniki ikionesha kuwa, baba wa mtoto
anaitwa Costa Haule. Huyu hana nia njema na mtoto kwani alitaka kumuua
kwa hiyo baada ya kumtibia tunawatafuta ndugu wa mwanaume au baba wa
mtoto ili wamlee wakati tukiandaa utaratibu wa kumfikisha mahakamani,”
alisema Afande Tausi.
GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment