Rais wa hivi sasa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dk Mahmoud Ahmadinejad
amekutana na rais-mteule Sheikh Hassan Rohani na wamejadiliana suala la
kuundwa kamati itakayosimamia makabidhiano ya madaraka.
Katika mkutano huo uliofanyika hapa Tehran leo asubuhi, Rais Ahmadinejad
kwa mara nyingine amempongeza Hassan Rohani kwa ushindi wake katika
uchaguzi wa rais uliofanyika Ijumaa iliyopita na kumtakia mafanikioa
katika jukumu hilo zito.
Rais Ahmadinejad amesema, serikali yake inayomaliza mihula miwili iko
tayari kushrikiana na rais mteule ili kumpa uzoefu iliyoputapa. Baada ya
kumalizika kikao hicho, Rais Ahmadinejad amesema, mazungumzo yake na Dk
Rohani yalikuwa mazuri.
Kwa upande wake, Rais-mteule Rohani ameshukuru Rais Ahmadinejad kwa
kumtembelea na kusema kwamba, fursa hiyo ilikuwa nzuri kwa ajili ya
kutathmini hali ya kiuchumi na kisiasa nchini Iran pamoja na
kubadilishana mawazo.
Rohani amesema, kipindi hiki cha mpito kinahitaji ushirikiano wa karibu.
Ameongeza kuwa, serikali ijayo itatumia uzoefu wa serikali inayoondoka
na hivyo uhusiano wa pande mbili utaendelea. Serikali ya duru ya 10 ya
Rais wa Iran iliyoongozwa na Dk Ahmadinejad itamaliza muhula wake rasmi
Agosti 3 mwaka huu, wakati ampapo Sheikh Hassan Rohani atakabidhiwa
rasmi hatamu za uongozi.
Rohani alichaguliwa kuwa rais wa Iran katika uchaguzi uliofanyika Ijumaa
ambapo alipata asilimia 50.7 ya kura milioni 36,704,156.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment