shekh Timondo mohamed said
Shekh wa Tumondo Mohamed Omary Said, amemwagiwa tindikali na mtu
asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na
jicho kuumia pia.Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mukhadam Khamis, amesema chombo kilichotumika kummwagia tindikali Shekh huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Shekh huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment