Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Naibu Spika, Job Ndugai.Dodoma, Tanzania. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amelazimika kuahirisha Bunge tena  hivi punde baada ya Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje kukataa kukiomba radhi chama cha CUF kwa kukihusisha na masuala ya ushoga na usagaji.

Baada ya Bunge kuahirishwa asubuhi kutokana na kauli ya Wenje, jioni hii, Mbunge huyo wa Nyamagana mkoani Mwanza ameshinikizwa tena na Mbunge wa CUF Jimbo la Mtambile, Masoud Abdallah Salim kuondoa maneno yanayozungumzia ushoga na usagaji na pia akiombe radhi chama cha CUF, lakini amekataa kuomba radhi.

Pia Ndugai alipomsisitiza tena Wenje kwa mara ya tatu aondoe maneno hayo na kuomba radhi, Wenje alikubali kuruka sehemu kwenye hotuba inayozungumzia ushoga na usagaji na kuendelea kusoma hotuba yake na kugoma kuomba radhi.

Kutokana na msimamo huo wa Wenje,  Naibu Spika amelazimika kuahirisha Bunge mpaka kesho tena na kuendelea bajeti ya wizara nyingine.

Awali Kamati ya Maadili ilikaa mchana kuzungumzia suala hilo na kumtaka Wenje kufuta, lakini hakukubali kufanya hivyo.


Kwa hisani ya Habari Masai

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top