Home
»
»Unlabelled
» MSHUHUDIE MAMA HUYU ALIYE JIFUNGUA WATOTO WATANO , HUKO SONGEA...................
Bi Jane Mlelwa aliyekaa kitandani akiwa amebeba mmoja wa wawatoto
watano aliowazaa kabla ya watototo hao kufa wote
Hawa ndio watoto aliojifungua katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na kesho wakafaliki dunia (Picha na maktaba)
..........................................................................
Akizungumza na Demashonews kwa njia ya simu Sophia Mgaya akiwa nyumbani kwake Ruhuwiko mjini
Songea alisema alilazimika kuomba kutoka wodini kwa sababu alikuwa akijisikia
uchungu anapowaona wanawake wenzake wodini humo wakiwakumbatia watoto wao baada
ya kujifungua huku wa kwake wote wakiwa wamefariki dunia baada ya kuzaliwa.
Alisema kuwa muda
wote aliokuwa hospitalini hapo baada ya watoto wake kufariki huku akiwa bado
anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa alikuwa akilia muda wote anapowaona
wanawake wenzake waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao hivyo
akaamua kuomba aruhusiwe kutoka hospitalini hapo.
‘’Niliomba
kuruhusiwa kutoka hospitali na kwenda kujiuguza kidonda nyumbani kwa sababu ya
uchungu na majonzi niiiyokuwa nikiyapata wodini hapo ninapowaona wanawake
wenzangu waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao huku wa
kwangu wakiwa wameshazikwa”alisema Bi.Mgaya
Aidha aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo pamoja na
wafanyakazi wote kwa namna walivyomuhudumia yeye pamoja na watoto wake watano
waliozaliwa na kuishi kwa muda wa masaa ya kumi ambapo alisema kuwa yote
yaliyotokea anaamini kuwa ni mapenzi ya Mungu.
Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma
Dkt.Benedict Ngaiza akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu kuwa waliamua
kuridhia ombi la mama huyo kuondoka hospitalini hapo baada ya kujiridhisha kuwa
anaendelea vizuri kwa sababu walifanya kila walichoweza kukoa uhai wake na
watoto lakini watoto walifariki baada ya masaa kumi.
Wakizungumza baadhi
ya wananchi waliomshuhudia mama huyo na watoto wake baada ya kuzaliwa na kabla hawajafariki walisema kuwa kuna kila
sababu kwa kila mwenye uwezo wa kumsaidia mama huyo kwa namna yoyote afanye
hivyo
Bi.Marietha Ngonyani
na Lusi Haule wakazi wa mjini Songea waliwaomba wananchi mbali mbali kujitolea
kumsaidia mama huyo kwa sababu bado anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa
na pia tukio hilo
limemuathiri kisaikolojia pia hivyo anahitaji faraja.
KWA HISANI YA Demashonews
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Recent Posts
- TCU IMESHUSHA SIFA ZA DIPLOMA KUJIUNGA DIGRII 2016/2017,SASA G.P.A16 Sep 20160
The Tanzania Commission for Universities (TCU) through the earlier public notice issued on 11th J...Read more ?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 9 201609 Sep 20160
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo September 09 201...Read more ?
- Mambo 10 Ambayo Mwanaume Hupenda Kusikia Toka Kwa Mpenzi Wake09 Sep 20160
10. Kukosolewa – “I think you are wrong”Wanaume wanaweza kujikweza sana lakini daima hawachukii ku...Read more ?
- Alikiba Aelezea ‘King Kiba’ ilikotokea, Adai si Mtu wa Maringo09 Sep 20160
Alikiba ametoa ufafanuzi wa wapi #KingKiba ilitokea kiasi cha kuitumia katika sehemu nyingi.Akiong...Read more ?
- VIDEO: Mama Wema Aeleza Beef yake na Man Fongo Kisa……..09 Sep 20160
NI Mama Wema Sepetu ambae ameingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutofautiana na mkali wa ...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment