Mrisho Ngasa akiongea na waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga baada y akutambulishwa rasmi jana
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)
Mrisho Ngasa akikabidhiwa jezi ya klabu ya Yanga na katibu mkuu Lawrence Mwalusako
Amesaini kadandalasi ya miaka miwili kuichezea yanga akitoka kwa wapinzani wao simba
MRISHO Ngassa jana Jumatatu kafunga kazi.Katambulishwa mbele ya
waandishi wa habari rasmi kwamba yeye ni mchezaji wa Yanga na kaibusu
jezi ya Yanga mbele yao. Kama kusaini alishasaini zamani kabla Sir Alex
Ferguson hajastaafu Manchester United au kabla Francis Cheka hajapigana
na Thomas Mashali
Amefanikisha alichokuwa anakitaka. Siku zote
anataka kucheza Yanga. Ndio timu ya damu yake. Ndio timu ya akili yake.
Ndio timu ya ngozi yake. Ndio timu ya nywele zake. Haifikirii West Ham,
Libolo, El Marreikh, Seattle Sounders wala Manchester United. Lugha
rahisi ni kwamba amepata alichotaka. Hongera nyingi kwa Ngassa.
Kikubwa zaidi ni kwamba wakati utatuambia. Mungu
akitupatia pumzi mpaka nyakati hizo tutakutana uzeeni na kujadili kwa
kirefu majuto ya maisha yetu. Wakati huo hatutotaka kusikia lawama wala
manung’uniko na masikitiko ya kukosa kucheza Ligi Kuu England. Tutakuwa
bize na wachezaji wengine.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment