CHAMA cha CUF na Chadema hivi punde Bungeni , vimekubali
kuomba radhi kutokana na vurugu zilizosababishwa na CUF yenye mrengo wa
Kiliberali na Chadema imemafanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na
masuala ya ushoga na usagaji.
Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge
kufanya kikao kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 2:30 usiku na kukubaliana
kila chama kumuomba spika radhi na pia kuliomba Bunge radhi kutokana na vurugu
za jana.
CUF wamelazimika kumuomba spika
radhi; kuomba radhi Bunge na kuwaomba radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje wakati
akisoma hutuba yake ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa Kiliberali
ambazo pamoja na mambo mengine ni ushoga na usagaji.
Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF, Rashidi wakati akiomba radhi
aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema kwa kufikia muafaka kwa maslahi ya
Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za
jana,” amesema hivi punde Rashidi.
Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya Upinzani Bungeni, Freeman
Mbowe amesimama Bungeni hivi pinde na kuwaomba radhi CUF, Bunge na Spika kutokana
na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni jana na Wenje.
Awali kabla ya kuomba radhi leo, Freeman Mbowe jana kwenye kikao
cha Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema kwamba CUF wanafuata mrengo wa
Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni shoga na usagaji na kwamba hawakufanya
kosa, pia alisema CUF alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF walichana hotuba yao
na kuwaudhi na kuwakera Chadema.
Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambali
wamelifanya leo asubuhi.
Wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo John Chiligati ambaye
ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki amesema jana CUF walikiri kwenye kamati
hiyo kwamba wao ni wanachama wa mrengo wa Kiliberali, lakini chama chao
hakikubaliani na sera zote kama za ushoga na usagaji kwa kuwa serikali
imeshatoa msimamo kwamba haiungi mkono masuala hayo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment