Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


23F3974F00000578-2869033-image-a-58_1418245346449
Hatua ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ilimalizika usiku wa Jumatano ikishuhudia michezo nane ambayo ilipigwa kwenye viwanja tofauti barani humo.
Katika michezo iliyopigwa siku hiyo Fc Barcelona walijihakikishia ushindi wa Kundi ‘F’ baada ya kuwafunga mabingwa wa Ufaransa, PSG kwa matokeo ya 3-0.
PSG ndio walioanza kufunga kwenye mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic bao ambalo halikudumu kwa muda mrefu kwani Lionel Messialisawazisha.
Kipa wa PSG akiruka bila mafanikio akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Neymar.
Kipa wa PSG akiruka bila mafanikio akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Neymar.
Barca hawakuishia hapo kwani dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika walifunga bao la pili safari hii mfungaji akiwa Neymar.
Kazi katika usiku mzuri kwenye uwanja wa Nou Camp ilimalizwa na mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez aliyefunga bao la tatu .
Matokeo haya yanawafanya Barcelona kufuzu kama washindi wa kundi lao huku PSGnao wakifuzu kama washindi wa pili.
Kwingineko Manchester City wakiwa ugenini kwenye mji mkuu wa Italia walifanikiwa kuwafunga As Roma 2-0 ushindi ambao umewapa tiketi ya kufuzu hatua ya 16 bora kama washindi wa pili kwenye kundi lao nyuma ya Bayern Munich.
Man City walifunga kupitia kwa Samir Nasri na Pablo Zabaleta ushindi uliowafanya wafikishe pointi nane.
Samir Nasri akishangilia na wenzie baada ya kuifungia Manchester City bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya As Roma.
Samir Nasri akishangilia na wenzie baada ya kuifungia Manchester City bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya As Roma.
Katika michezo mingine Ajax Amsterdam waliwafunga Apoel Fc 4-0 , Chelseawaliwafunga Sporting Lisbon 3-1, Fc Schalke wakashinda dhidi ya NK Maribor kwa matokeo ya 1-0 , Athletic Bilbao wakawafunga Bate Borisov 2-0 na Fc Porto naShakhtar Donetsk wakatoka sare ya 1-1,Bayer Munich waliifunga CSKA Moscow 3-0.
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia moja kati ya mabao matatu waliyofunga dhidi ya Sporting Lisbon .
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia moja kati ya mabao matatu waliyofunga dhidi ya Sporting Lisbon.
Kwa matokeo haya timu za Barcelona , PSG , Chelsea , Schalke, Bayern Munich , Manchester City , Fc Porto na Shakhtar Donetsk zimefuzu hatua ya 16 bora zikiungana na timu zilizofuzu hapo jana ambazo ni Real Madrid, Fc Basle, Atletico Madrid, Juventus, Borusia Dortmund, Arsenal, Monaco na Bayer Leverkusenkatika hatua ya 16 bora ambayo ratiba yake itapangwa jumatatu ijayo .

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top