Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MASHABIKISIMBA
Ligi kuu ya soka ya Tanzania bara imerejea hii leo baada ya mapumziko ya mwezi mmoja na nusu wakati ligi hiyo iliposimama .
Katika mchezo uliopigwa hii leo , wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club walianza vibaya nusu ya pili ya mzunguko wa kwanza baada ya kukubali kipigo cha bao moja bila .
Bao hilo pekee lilifungwa kwenye dakika ya 21 na  mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Coastal Union Atupele Green ambaye alifanyia kazi makosa ya kipa wa Simba Ivo Mapunda na beki Mohamed Hussein .
Kwa matokeo haya Kagera Sugar wamefikisha pointi kumi na tatu baada ya michezo nane na wanapanda mpaka kwenye nafasi ya nne .
Ligi hiyo itaendelea hapo kesho kwa michezo miwili ambapo Jkt Ruvu na Ruvu Shooting watacheza huko Azam Complex Chamazi , na Tanzania Prison watacheza na Coastal Union huko Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top