Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Staa wa Filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.

Staa wa Filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameibuka na kusema kuwa kuelekea mwisho wa mwaka mastaa wengi wana ngoma na mbaya zaidi wanaambukizana wao kwa wao.
Akizungumza na Ijumaa, Dude alisema kuwa mastaa wazima ni wa kuhesabika na kutaja sababu kubwa kuwa ni kubadilishana na kuibiana wapenzi bila kuwa na woga . 
“Utakuta Mbongo Fleva ana mtu kwenye Bongo Muvi na Mbongo Muvi ana mtu kwenye dansi au kwa mamis au hata wacheza mpira, ukitaka kuujua ukweli tangaza dau kuwapima mastaa uone watakaojitokeza,” alisema Dude. Aidha, Dude alisema anavyoona yeye ingeanzishwa kampeni ya mastaa wa Bongo kupima Ukimwi kwani anawahofia watoto wa kizazi kipya zaidi ambao wanajikuta wanaingia pabaya na kuzima ndoto zao.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top