Di Maria, ameshinda tuzo hiyo baada ya kupigiwa kura na mashabiki wa klabu ya Man utd kwa asilimia kubwa tofauti na wachezjai wengine ambao walikuwa kwenye orodha ya kinyang’anyirio hicho baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo ya mwezi uliopita.
Kigezo kikubwa kilichompa tuzo hiyo kwa urahisi kutoka kwa mashabiki wa Man Utd, ni uwezo na mchango wake aliouonyesha tangu aliposajiliwa klabuni hapo ambapo mpaka sasa ameshacheza michezo mitatu na kufunga mabao mawili.
Di Maria ameshinda kwa asilimia 68 ya kura zote za mashabiki zilizopigwa, hatua mbayo ni kubwa sana kwake kutokana na muda mfupi aliokaa klabuni hapo akitokea nchini Hispania.
Wachezaji wengine waliokuwa wanashindanishwa na Di Maria katika kinyang’anyiro hicho ni Ander Herrera aliyepata asilimia 23 ya kura pamoja na Rafael aliyepata asilimia 9.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment