Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MWIGIZAJI kiwango enzi hizo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ aliyepotea kwa muda, ameibukia kwenye Runinga ya EATV na kumbutua staa wa mwenzake, Kajala Masanja kwamba, anatumia nafasi ya kuonekana kwenye filamu kujipatia wanaume kama si mabwana!
Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Mkasi kinachoratibiwa na Mtangazaji Salama Jabir, Jumatatu iliyopita, Nora alisema fani ya uigizaji imevamiwa kwa sasa kwani kuna watu ambao wanaingia kwenye gemu ili wauze sura na kuonekana na wanaume wapate ‘soko’ kiulaini.
Aliongeza kuwa, watu hao kupitia vitendo hivyo wamekuwa wakiichafua tasnia kiasi cha wote kuonekana hawafai (samaki mmoja akioza, ni wote).
Nora alikwenda mbali zaidi alipoulizwa na Salama ni nani na nani hawafai na nani wanafaa, alishindwa kuwataja kwa majina moja kwa moja lakini mtangazaji huyo akaomba ataje majina yeye kisha Nora aseme kama anafaa au hafai!
Salama: “Kajala.”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Batuli.”
Nora: “Huyo pia hamna kitu.”
Salama: “Lulu.”
Nora: ”Huyo safi.”
Mwigizaji kiwango enzi hizo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’.
Salama: “Mlela (Yusuf).”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Steve Nyerere.”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Hemed (Suleiman).”
Nora: “Hamna kitu hapo.”
Juzi gazeti hili lilimsaka Kajala kwa njia ya simu hakupatikana, lakini mmoja wa watu wake wa karibu alisema staa huyo ameshangaa sana Nora kutaka kurudi juu kwa kutumia jina lake.
“Kajala amezima simu, lakini kamshangaa sana Nora, alishazimika, sasa anaonekana anataka kuwaka tena kwa kutumia jina lake,” alisema mpambe huyo.
Bonyeza Hapa like page yetu

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top