Dar es Salaam, Tanzania. Mahakama ya Kuu yaTanzania, Kanda ya Dar es Salaam hivi punde imetupilia mbali maombi ya pingamizi la awali la kusimamisha Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma baada ya kesi hiyo kufunguliwa na Mwandishi wa Habari Said Kubenea kwa kwa sababu ametumia kifungu cha sheria ambacho siyo sahihi.
Kesi hiyo imetupiliwa mbali kwa sababu mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA) ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.
Uamuzi huo umetolewa chini ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Augustino Mwarija, Aloyisius Mujuluzi na Dk Fauz Twaib.
Bonyeza Hapa like page yetu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment