Zikiwa ni takribani wiki tatu tangu tasnia ya muziki wa injili nchini kumpoteza mmoja wa waimbaji wake marehemu mchungaji Debora Saidi, taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba mwimbaji mwingine wa muziki wa injili Orida Njole amefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Orida ambaye mpaka umauti unamfika mchana wa leo ilikuwa bado haijajulikana nini hasa kinamsumbua lakini alikuwa ameishiwa damu sana, mpaka umauti unamkuta alikuwa anatamba na album yake iitwayo 'Duniani tu wapitaji' huku kwa mujibu wa watu waliomfahamu marehemu wameeleza kwamba alikuwa mtu mchangamfu wakati wote wakati wa uhai wake na kwamba wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe!
![]() |
| Picha ya mbele ya álbum ya marehemu Orida Njole. |
![]() |
| Marehemu Orida akiwa na mtoto yatima katika kituo cha Tosamaganga Iringa alipotembelea kituoni hapo
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa
|
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro









Post a Comment
Post a Comment