Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

                        Wapiganaji wa Boko Haram
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch linasema kuwa zaidi ya raia 2,000 wameuawa nchini Nigeria mwaka huu na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Kwa mujibu wa shirika hilo, vifo hivyo vimetokea katika mashambulizi 95 tofauti katika zaidi ya miji 70 na vijiji kaskazini mashariki mwa taifa hilo.

Rais Goodluck Johnathan amepata shinikizo la kusitisha mashambulizi hayo na kuwaokoa zaidi ya wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara miezi mitatu iliopita.

Anatarajiwa kukutana na baadhi ya familia za wasichana hao kufuatia ombi la mwanaharakati wa Pakistan Malala Yousafzai ambaye alikutana naye hapo jana.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top